Viongozi mbalimbali wa Serikali wameonya watu wanaotumia vibaya mitandao kuzusha taarifa zinazozusha taharuki miongoni mwa jamii.

Viongozi hao ni pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ambaye kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameandika “Asante Viongozi mbalimbali wa kitaifa/kijamii kupitia kurasa za Twitter na Instagram kuonesha kutopendezwa uvumi wa nia pvu kuleta taharuki ndani ya nchi yetu…….”

Naye Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba ameandika, “Kiongozi wa Nchi sio Parishworker Kanisani wala sio Mzee wa Kanisa kwamba alipangiwa zamu na hakuonekana!, Kiongozi wa Nchi Sio Mtangazaji wa TV kwamba alikuwa na kipindi Ila hakuonekana! Kiongozi wa Nchi sio kiongozi wa jogging clubs kwamba anatakiwa kuwa tu mtaani kila siku na kurusha selfie…. SHERIA YEYOTE INAPOVUNJWA, HAKUNA CHA MIPAKA, WALA HAKUNA CHA MUDA KUPITA. KWA WANAOROPOKA ZINGATIENI KIFUNGU CHA 89 cha Penal code na 16 cha Cyber Crime, SERIKALI IPO KAZINI.”

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Hamisi Taletale maarufu Babu Tale kupitia ukurasa wa wa Instagram ameandika “Nawashangaa sana wanaosambaza uvumi usio na utu, heshima na nidhamu dhidi ya kiongozi mkuu wa nchi yetu. Eti kwa nini hakuonekana kwenye Ibada Jumapili iliyopita, kwani Mhe. Rais huwa anaonekana kila Jumapili? Mimi ni Mtanzania ninayefuatilia taarifa za Rais wangu bila kukosa, sio Jumapili zote hutolewa taarifa za Rais kuhudhuria Ibada ya Jumapili.

Pili, nimeshangaa sana majirani zetu wanavyoingia kichwakichwa kwamba Rais wetu kaenda kutibiwa maradhi ya moyo na Korona katika hospitali moja ya Nairobi. Hivi kama Rais anatafuta rufaa ndio apelekwe Nairobi? Yaani Rais aache kwenda Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambayo ni moja ya vituo bora Afrika kwa kutibu maradhi ya moyo aende Nairobi? Wakati Wakenya kibao wanakuja kutibiwa Moyo Tanzania. Acheni hizo.

Mhe. Rais wewe chapa kazi, hawa tutajibizana nao sisi, wewe wala usihangaike nao, wala Serikali msihangaike nao. Bahati nzuri wanaoendesha ajenda hii ni Watanzania wenzetu na tunawajua, na tunajua sasa hivi hawana hoja wamebaki kusingizia watu kufa na kubangaiza hoja kupitia ugonjwa wa Korona.

Tunaendelea kukuombea Rais wetu, Mungu akupe afya njema, busara na hekima ya kuendelea kuliongoza Taifa letu,” ameandika Babu Tale.

Hatua hii ya Viongozi inafuatia kusambaa kwa taarifa za uvumi katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu hali ya afya ya Rais Magufuli.

Wakamatwa wakisafirisha nyoka na vinyonga
Waziri Mkuu wa Ivory Coast afariki dunia