Suala la utafutaji wa amani, kimetajwa kuwa ni mchakato muhimu na wa lazima, ukiwa kama njia pekee ya vitendo kuelekea ulimwengu bora na wa haki kwa watu wote huku uhimizwaji wa kuepuka mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ukisisitizwa na badala yake kuunganisha nguvu za pamoja kumkabili adui.

Kupitia ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya amani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema “Lakini bado katika maeneo mengi, katika mazingira mengi sana, tunashindwa katika suala la amani na ikiwa tutaunganisha nguvu sisi sote tutamshinda adui yetu tuepuke kupigana wenyewe.”

Guterres ameongeza kuwa “Ubaguzi wa rangi unawanyima watu haki na utu wao. Unachochea ukosefu wa usawa na kutoaminiana. Na unawatenganisha watukatika wakati ambapo tunapaswa kuwa tunashikamana pamoja, kama familia moja ya kibinadamu, kurekebisha ulimwengu wetu uliopasuka.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres. Picha na UN.

Aidha ameendelea kusisitiza kuwa, “Badala ya kupigana sisi kwa sisi, tunapaswa kufanya kazi ili kuwashinda maadui wetu wa kweli ambao ni ubaguzi wa rangi, umaskini, ukosefu wa usawa, migogoro, changamoto za tabianchi na janga la Uviko-19 sote tunapaswa kubomoa miundo inayoendeleza ubaguzi wa rangi, na kuinua harakati za kupigania haki za binadamu kila mahali.”

Kaulimbiu ya siku ya kimataifa ya amani ya mwaka huu ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 21 ni, “Komesha ubaguzi wa rangi, jenga amani” ikikumbusha njia nyingi za ubaguzi wa rangi kama mbinu muhimu ambayo hutia sumu mioyo, akili za watu na kuharibu amani ya ulimwengu inayotafutwa.

Hata hivyo, Katibu Mkuu amehitimisha ujumbe wake kwa kusema, “Katika siku hii muhimu, wakati wa kuzingatia saa 24 za kutokuwa na vurugu na kusitisha uhasama tunasisitiza wito wetu kwa watu wote kufanya juhudi zaidi zaidi ya kuweka chini silaha zao na tunatoa wito kwao kuthibitisha vifungu vya mshikamano na kufikia mchakato wa kujenga ulimwengu bora na wa amani.”

Wenye uziwikutoona waiangukia Serikali
Wizara ya Afya yatahadharisha ugonjwa wa Ebola