Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mojawapo ya ajenda za kitaifa ni kudhibiti mmomonyoko wa maadili na ukatili dhidi ya wanawake na watoto na amewataka viongozi kusimamia suala hilo kwa karibu zaidi.

Majaliwa ameyasema hayo mwishoni mwa wiki na kuongeza kuwa, “twende tukasimamie suala la mmomonyoko wa maadili na ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kwani hivi sasa kuna vitu vinaingia ambavyo si desturi na mila zetu. Makamu wa Rais amelieleza suala hili vizuri wakati akiwa kwenye Kanisa mojawapo.”

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema, “tumeanza kuona kuna vitabu vinapenyezwa hadi shuleni. Maafisa Elimu na wakaguzi nendeni mkafanye ukaguzi, vitabu ambavyo havijachapishwa au kupitishwa na taasisi yetu, ili vitumike kwenye syllabus zetu vitoeni, visiingie humo.”

“Kuna suala la mabweni, tembeleeni mkague mabweni kama ni ya wasichana pekee na wavulana peke yao ili wanaoingia huko wasije kutumia mwanya huo. Kaeni na wakuu wa shule wasimamie sana eneo hilo na kuhakikisha kuna patron na matron kwa kila bweni,” amesisitiza Waziri Mkuu.

Upandaji miti ni zoezi endelevu: Makamu wa Rais
Miradi umwagiliaji iboreshe hali za Wakulima: Mavunde