Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz na Mkurugenzi wa mashtaka nchini(DPP), Biswalo Mganga wamewasili katika Kisiwa cha Ukara, Ukerewe, mkoani Mwanza kufanya uchunguzi ili kuwabaini wanaotenda uhalifu uliopelekea mauaji ya watu wawili kisiwani hapo.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kushamiri kwa vitendo vya uhalifu katika kisiwa cha Ukara kilichopo wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, hali iliyopelekea wakazi wa kisiwa hicho kuishi kwa wasiwasi.

DCI Boaz na DPP Mganga wamefika katika kijiji cha Bukungu kilichopo katika kisiwa hicho na kuwatoa hofu wakazi hao.

Viongozi hao wameambatana na mwenyeji wao Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Muliro Jumanne ambaye ameahidi kuwa mauaji hayo yatakomeshwa.

Madereva bodaboda, bajaji fuateni sheria kipindi cha Uchaguzi
Waziri mkuu kujiuzulu kutokana na sababu za kiafya - Japan