Serikali nchini, imetoa maelekezo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha vibali vya ujenzi vinavyotolewa kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya wananchi vinaelekeza wajibu wa mwananchi kupanda idadi ya miti katika eneo husika ili kulinda mazingira.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo na kuongeza kuwa Serikali pia imetoa maelekezo kwa Mamlaka za Serikali
za Mitaa kuhakikisha vibali vya ujenzi vinavyotolewa kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya wananchi
vinaelekeza wajibu wa mwananchi kupanda idadi ya miti katika eneo husika.

Amesema, “Takribani miti Milioni 276 itapandwa kila mwaka, na hili ni lengo la kila Halmashauri kupanda miti Milioni 1.5 kila mwaka, kwa hapa Dodoma lengo ni kupanda Miti Milioni 40 ambalo ni lengo la kipekee ukilinganisha na Mikoa na Wilaya nyingine nchini. Tunazishukuru Mamlaka za
Serikali za Mitaa kwa kusimamia vyema kampeni hizi.”

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameishukuru Ofisi ya
Makamu wa Rais kwa kuendelea kuipatia ushirikiano ofisi yake kwa kuendelea kutoa msukumo
na hamasa ya uhifadhi wa utunzaji wa mazingira kupitia Mpango Mkakati wa Mazingira ambapo
Mkoa wa Dodoma umetajwa kama Mkoa pekee uliowekewa shahada ya uhifadhi wa mazingira.

Shambulizi mpakani lauwa 12, Jeshi laomba msaada
Simba SC yapigwa bao Afrika Kusini