Mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara kati ya Yanga na Mwadui FC umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa Mabao 2-1 kwenye mchezo ulioanza kwa Yanga kuishambulia Mwadui kwenye dakika za mwanzoni.

Kwenye mchezo huo mabao ya Yanga yamewekwa kimiani na winga wake mwenye kasi Simon Msuva kwenye dakika ya 3 ya kipindi cha kwanza baada ya kuitumia vizuri krosi iliyoelekezwa kwenye lango la Mwadui.

Baada ya bao hilo Mwadui walicharuka na kulisakama lango la Yanga na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 14 kupitia kwa Kelvin Sabato baada ya gonga gonga zilizopelekea Thabani Kamusoko kufanya makosa yaliyosababisha bao hilo.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa suluhu ya mabao 1-1. Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana ingawa Yanga walionekana kupeleka zaidi mashambulizi langoni mwa Mwadui.

Mnamo dakika ya 71, Mwadui walipata pigo baada ya Iddy Mobby kuoneshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje na mwamuzi wa Selemani Kinugani wa Morogoro.

Yanga walitumia walitumia vizuri upungufu wa Mwadui kusaka bao la ushindi lililopatika dakika tatu kabla ya muda wa kawaida kutimia. Shuti la kimo cha chini kutoka kwa kiungo Haruna Niyonzima lilimpita kipa Shaban Kado na kutinga nyavuni.

Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Morogoro, Azam wamefanikiwa kuibuka na pointi tatu muhimu baada ya kuwafunga wenyeji Mtibwa Sugar bao 1-0.

Nahodha John Bocco ndiye mfungaji wa bao hilo muhimu kwa Azam inayoshikilia nafasi ya tatu.

ZFA Kuwapata Viongozi Wapya Hii Leo
Leicester City Wachomoza Kivingine England