Meneja wa klabu ya Everton Ronald Koeman ameweka dhamira ya kumsajili kwa mara ya pili beki kutoka nchini Uholanzi Virgil van Dijk.

Koeman alimsajili kwa mara ya kwanza beki huyo, alipokua mkuu wa benchi la ufundi la Southampton, akimtoa Celtic ya nchini Scotland kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 13.

Gazeti la The Daily Mirror limeripoti kuwa, Koeman anaamini usajili wa Van Dijk utamaliza kiu ya kuboresha safu ya ulinzi ya Everton.

Sababu kubwa ya Koeman kumuhitaji Van Dijk ni kutaka kuziba pengo lililoachwa wazi na John Stones, ambaye mwanzoni mwa msimu huu alijiunga na Man City.

Mipango ya usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 25, huenda ikakamilishwa mwezi januari mwaka 2017, wakati wa dirisha dogo la usajili, lakini The Saint wamedai kuwa tayari kumuachia Van Dijk kwa ada ya Pauni milioni 40.

Homa Ya El Clasico Yamtesa Gerard Piqué
Berlusconi: AC Milan Tayari Imeshauzwa