Bosi wa kikosi cha Southampton Claude Puel, amemtaka beki wake kutoka nchini Uholanzi Virgil van Dijk kuzipuuza taarifa za kuwindwa na klabu za Liverpool na Everton.

Van Dijk ambaye tayari thamani yake imetajwa kuwa Pauni milioni 40, amekua na kiwango kizuri katika safu ya ulinzi ya The Saint, hali ambayo imezivutia klabu za Merseyside (Liverpool na Everton).

“Van Dijk ni mchezaji mkubwa na mwenye kiwango kwa sasa,” alisema Puel. “Lakini pia ana mkataba na klabu ya Southampton na litakua jambo la umuhimu kwake kuuheshimu mkataba huo ili aendelee kufanya kazi akiwa hapa.

“Ninapendezwa na uwezo wa Virgil, amekua akifanya vizri wakati wote tangu msimu huu ulipoanza, na wakati mwingine hufanya kazi ya ziada kwa ajili ya kuisaidia timu.

“Sioni sababu ya kuanza kujipa mawazo ya kutaka kusajiliwa na klabu nyingine ambazo zinatajwa katika vyombo vya habari, nimemshauri afute mawazo hayo na badala yake aongeze bidii ya kuisaidia Southampton ili ifikie malengo yake.”

Mathieu Debuchy Asukiwa Mipango Ufaransa
West Ham Utd Kumfungia Kazi Payet