Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema litafanya mkutano wa dharura kesho jijini Geneva ili kutathmini kama maambukizi ya virusi vya Korona vya aina mpya yanayotokea hivi karibuni nchini China ni tukio la dharura la afya ya umma duniani au la. WHO imeeleza kuwa baada ya tathmini watatoa ushauri juu ya jinsi ya kudhibiti maambukizi hayo.

Mwakilishi wa WHO nchini China, Dkt. Gaduden Galea leo, Januari 21, 2020 amesema kutokana na safari nyingi zinazofanywa na watu wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa Jadi wa Kichina itakayoanza wikiendi hii na ongezeko la vipimo katika hospitali, huenda maambukizi ya virusi hivyo vya Korona yataongezeka ndani na nje ya China katika siku zijazo.

Dkt. Galea amesema takwimu mpya zimeonyesha wazi kuwa virusi vipya vinaweza kusababisha maambukizi kati ya watu na watu na kesi za kuambukizwa kwa wauguzi ni ushahidi. Hata hivyo, amesema wanahitaji kufanya uchambuzi zaidi kuhusu takwimu za magonjwa ya kuambukizwa ili kujua kasi ya maambukizi.

WHO imeushauri umma kuongeza hatua za afya ya umma na kuongeza usalama wa chakula ili kupunguza hatari ya kugusa na kuambukiza magonjwa ya aina hiyo.

TCU yafuta vyuo tisa, kimo chuo kikuu na vyuo vikuu vishiriki
Video: Makonda amfunda, Samatta, TFF wataja majukumu yake