Serikali ya Kenya leo, Mei 13, 2020 imetangaza visa vipya 22 vya corona na kufanya visa vya corona nchini humo kufika 737.

Visa hivyo vimeainika baada ya kufanya vipimo vya sampuli 1,516 ndani ya saa 24, vilivyojumuisha Wakenya 21 na raia mmoja wa Uganda.

Hadi leo, Kenya imefanya vipimo vya sampuli 35,432 tangu kutangazwa kwa mlipuko wa virusi vya corona mwishoni mwa mwaka 2019. Kisa cha kwanza kiliripotiwa nchini humo Machi mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya, waliopatikana na virusi hivyo ni watu wenye umri kati ya miaka 20 na 81, wanaume 17 na wanawake watano.

Maeneo yaliyobainika kuwa na wagonjwa hao wapya ni Nairobi (10), Mombasa (8), Kajiado (3) na Bomet (1).

Katibu Mkuu wa Wazira ya Afya, Dkt. Rashid Aman amesema kuwa wagonjwa 22 waliruhusiwa kutoka hospitalini Jumatano, Mei 12, 2020 hatua inayofanya waliopona na kuruhusiwa kutoka hospitalini kufikia 281.

Mbowe na wenzake kutorejea Bungeni bila kutimiza Masharti ya Spika

Ayoub Lyanga: Young Africans hawatimizi ahadi, nitakwenda Serbia

Luc Eymael kuamua hatma ya Kaseke
Ayoub Lyanga: Young Africans hawatimizi ahadi, nitakwenda Serbia

Comments

comments