Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji wa mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA John Daffa amesema wana mpango wa kuondoa mafundi vishoka wa kutengeneza simu mtaani.

Daffa amesema kuwa hadi sasa wameshaanza kutoa leseni kwa watengenezaji wa simu ambao wamekidhi vigezo kutoka vyuo husika ambavyo ni VETA na Taasisi ya Teknolojia (DIT).

Sambamba na hilo TCRA ina mpango wa kujenga kiwanda cha kutengeneza simu nchini ili kurahisisha upatikanaji wa ajira kwa wahitimu kwa ngazi ya Ufundi Stadi na kufanya Usalama wa Mawasiliano.

Aidha ujenzi wa kiwanda hicho unatazamiwa kuanza mwakani 2021 ambapo wanufaika wakuu watakuwa ni wahitimu kutoka VETA.

Ntibazonkia: Msimu huu tutakuwa mabingwa
Vifo vitokanavyo na ajali vyapungua mwaka 2020