Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Monn anasema ana wasi wasi kwa kufuatia kuendelea kwa mapigano nchini Sudan Kusini.

Kumeripitiwa mapigano nje na ndani ya mji wa Wau, kati ya wanajeshi wa serikalia na makundi yaliyojihami tangu Ijumaa.

Haijulikani wapiganaji hao ni akina nani.

Mashirika ya kutoa misaada yanasema kuwa maelfu ya raia wamekimbia na pia kuna ripoti za uporaji na vifo.

Hali ni tete nchini Sudan Kusini licha ya kuundwa kwa serikali ya umoja, yenye lengo la kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza mwaka 2013

Vikosi vya Iraq vyawatimua wapiganaji kutoka Fallujah
Kujiondoa kwa Uingereza kutaathiri uchumi wa dunia