Shirika la Afya Duniani WHO, limetoa wito wa msaada zaidi wa kifedha ili kusaidia juhudi za kukabiliana na changamoto zinazozidi katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria unaowauwa maelfu ya watoto hasa kwa bara la Afrika.

Kupitia ripoti hiyo mpya, WHO imesema visa vya maambukizi na vifo vinavyotokana na malaria ambavyo vilikuwa vingi kwa mwaka 2020 wakati ambapo janga la Uviko-19 lililemaza juhudi za kinga na matibabu kwa mwaka jana (2021).

Hata hivyo, WHO imetahadharisha kuwa ulimwengu kwa sasa hauko katika njia sahihi ya kulifikia lengo la kupunguza visa vya malaria kwa asilimia 90 ifikiapo mwaka 2030.

Aidha, WHO pia inasisitiza kuwa ufadhili unastahili kuongezwa mara ya mbili ya ahadi zilizowekwa awali, ili kusaidia kufanikisha mapambano hayo na kuokoa mamia ya vifo vya watoto maeneo mengi Ulimwenguni.

Rais aliyeondolewa madarakani awekwa kizuizini
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Decemba 9, 2022