Mapigano kati ya wanajeshi wa FARDC nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 yanayondelea katika eneo la Nyiragongo karibu na Goma uliopo Kivu Kaskazini yamesababisha maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao.

Mapigano hayo yaliyoanza Mei, 24, 2022 yanadaiwa kusababishwa na vikosi hivyo viwili kinzani kutaka umiliki wa eneo la kimkakati ambalo liko karibu na mji wa Goma na yameleta adha kwa raia wanaokimbilia maeno jirani na Goma ili kuokoa maisha yao.

“Tumehama tunakimbia mapigano yaliyotokea leo na tunaogopa ndiyo maana tunakwenda Kibati karibu na Goma tuokoe maisha yetu,” amesema mkazi wa Nyiragongo Alexis Sikuli.

“Ningependa kumwambia Rais wetu Félix Tshisekedi kwamba tumechoshwa na vita tunaomba aangalie kutuokoa na mateso haya,” ametoa ujumbe wake raia Aline Mundozi.

Hata hivyo mamlaka za mitaa katika eneo hilo zinaamini kuwa shambulio la kijiji cha Buhumba limetokana na waasi wa kikosi cha upiganaji cha M23 waliotoka katika mpaka wa nchi ya Rwanda.

“Tunathibitisha bila kuogopa kupingwa kuwa ni Rwanda inayounga mkono M23 kwa sasa kwa sababu M23 walishashindwa na wasingekuwa na nguvu tena ya kuja kushambulia FARDC yetu shupavu,” amefafanua mwanachama. wa asasi za kiraia za mitaa Ghislain Bolingo.

Jumatatu Mei 23, 2022 jeshi la Rwanda lilishutumu vikosi vya DRC kufyatua mabomu katika ardhi yake na kuomba uchunguzi ufanyike juu ya tukio hilo madai yanayopingwa na msemaji wa gavana wa Kivu kaskazini anayesema hilo ni igizo lisilo na maana.

Kundi la M23 ni waasi wa zamani wa Watutsi walioshindwa mwaka 2013 na wanajeshi wa DRC ambao walitokea tena mwishoni mwa mwaka jana wakiishutumu mamlaka ya Kinshasa kwa kutokuwa na ahadi zinazoheshimiwa juu ya kuwaondoa wapiganaji wake.

Triple C atemwa Chipolopolo, Bwalya safi
Habari Kuu kwenye Magazeti leo Mei 25, 2022