Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe, Andrea Tsere anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika zoezi la uzinduzi wa shughuli ya ugawaji vitambulisho Kwa wafanyabiashara wadogo (Wajasiliamali) wilayani humo litakalofanyika January 3 Mwaka mpya 2019.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Sunday Deogratius ambapo amesema kuwa tayari Halmashauri yake imepokea Jumla ya Vitambulisho 2500 Tayari kwa kuwakabidhi wafanyabiashara wadogo wenye sifa stahiki ambao mauzo yao ni chini ya milioni Nne kwa Mwaka.

“Ndugu Mwandishi wa habari nikujulishe rasmi kuwa vile vitambulisho ambavyo Mh. Rais amevitoa kwa ajili ya wafanyabiashara tayari tumeshavipata ambapo sisi katika Halmashauri yetu ya Ludewa tumevipokea vitambulisho 2500 Kutoka ngazi ya mkoa ambapo tumeamua kuwatangazia wafanyabiashara wote wa Ludewa wafike Tarehe 03 Mwezi January Mwaka 2019 Ili tuwakabidhi Hata Wale ambao mitaji yao ni zaidi wafike ili waweze kuona Jinsi serikali yao inavyowasikiliza”. Alisema Bw. Sunday Deogratius Mkurugenzi Mtendaji (HW) Ludewa.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Biashara wa Wilaya ya Ludewa, Nicolaus Mchilo amesema kuwa mfanyabiashara mdogo atakayepata kitambulisho hicho ni yule ambaye mtaji wake upo chini ya Milioni nne kwa mwaka pia ambaye hajawahi Kusajiliwa au kupewa TIN namba na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Na kutambuliwa kama Mlipakodi Huku akisema Kuwa idara yake inaendelea Kutumia Njia mbalimbali ili kuwatambua Wafanyabiashara wenye vigezo hivyo.

Hata hivyo, Afisa Biashara huyo ameongeza kuwa baada ya kupata kitambulisho hicho Mjasiliamali huyo atalipa kodi ya biashara yake kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kiasi cha Tsh. 20,000/= Kwa mwaka bila kusumbuliwa.

Video: Lissu achafua hali ya hewa Chadema, Simbachawene ampa kichapo dereva wa lori
Moto wateketeza vyumba vinne Njombe

Comments

comments