Kuna faida mbalimbali zitokanazo na matumizi ya vitamin kiafya hasa katika urembo hususani katika vitamin C na Vitamin E ambazo huboresha muonekano wa ngozi yako.

Faida ya vitamin E katika ngozi hupunguza kasi ya ngozi kuzeeka, kupunguza madhara ya mionzi ya jua kwenye ngozi lakini pia hupunguza muonekano mbaya wa makovu na vipele.

Iwapo unataka kupunguza kupauka ngozi, madoa, makovu inashauriwa kuchanganya mafuta ya Vitamin E na maji ya limao katika mafuta unayoyatumia pia unaweza kuongeza rose water katika huo mchanganyiko.

Tumia pamba kupaka usoni na shingoni kaa na mchanganyiko huo kwa muda wa robo saa kisha safisha uso tumia kwa siku 7 hadi 10 kuona mabadiliko pia itakusaidia kutibu chunusi.

Unaweza kupaka usiku wakati wa kulala na asubuhi unasafisha uso wako kwa kuchanganya kijiko kimoja cha ya mzaituni au mafuta ya nazi na mafuta kidonge kimoja cha vitamini kisha unapaka kwa kuzunguka uso kwa kutumia vidole vyako.

Unashauriwa kutotumia mafuta ya Vitamin E bila ya kuchanganya na kitu chochote kuyapunguza nguvu kunaweza kukuletea mchubuko wa ngozi laini kama ya kuzunguka macho.

 

Fahamu vitu vitano kwenye simu vinavyomaliza chaji
Magufuli atuma rambirambi vifo vya waumini 20 kwa mafuta ya Mwamposa

Comments

comments