Hakuna binadamu aliyekamilika kila binadamu anamapungufu yake ambayo kwa namna moja au nyingine ni kikwazo kwa mtu mwingine, kukosea katika maisha ni sehemu ya kujifunza, kuonekana hujui jambo au kitu fulani ni sehemu ya maisha pia, hivyo usikate tamaa pale ambapo unakataliwa au unaonekana hufai.

Sasa leo nimekuandalia mambo 7 yanayopatikana katika maisha, mambo 4 yatakayokufanya uishi vizuri na watu wa aina yeyote, mambo 4 unayopaswa kuwa nayo, na mambo 5 unayopaswa kuyaepuka au kutokuwa nayo.

Maisha yana vitu 7

  1. Furaha
  2. Karaha
  3. Misukosuko
  4. Majonzi
  5. Migogoro
  6. Mikasa
  7. Chuki.

Mambo hayo katika maisha ambayo hayaepukiki unaweza kuyashinda kama utaweza kuwa mambo haya 4 muhimi

  1. Subira
  2. Uelewa
  3. Uvumilivu
  4. Msamaha

Pamoja na hayo inashauriwa ili uwe na hekima lazima uwe na mambo haya manne muhimu.

  1. Msimamo
  2. Mkweli
  3. Ujasiri
  4. Imani

Na hekima hiyo itazidi kukujaa kama utaepekana na mambo haya matano hatari zaidi.

  1. Udanganyifu
  2. Uchoyo
  3. Ubinafsi
  4. Wizi
  5. Kufitinisha

 

 

Wizara ya afya yatuma mtaalum kuchunguza mwili wa mwanafunzi aliyeuawa Bukoba
Claudio Marchisio azigonganisha FC Porto, SL Benfica