Jean Baptiste Mugiraneza wa Azam FC na Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima wa Young Africans wote wameitwa kwenye kikosi cha Rwanda kwa ajili ya michezo miwili ya Kundi H ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Mauritius itakayochezwa juma lijalo.

Kocha Muingereza, Jon McKinstry ametaja kikosi cha wachezaji 15 kilichofika hatua ya robo fainali ya michuano ya CHAN mapema mwaka huu mjini Kigali kati ya 26 wataoingia kambini mwishoni mwa juma.

Rwanda itapambana na Mauritius Jumamosi ya Machi 26 mjini Belle-Vue kabla ya kurudiana siku tatu baadaye mjini Kigali na Amavubi inatarajiwa kuingia kambini Jumamosi ya Machi 19 kuanza maandalizi ya mechi hiyo.

Rwanda ina pointi tatu sawa na Mauritius, wakizidiwa pointi tatu na vinara wa kundi hilo, Ghana wakati Msumbiji haina pointi na inashika mkia.

Kikosi kamili cha Amavubi kinaundwa na makipa; Eric Ndayishimiye (Rayon Sports), Olivier Kwizera (APR), Marcel Nzarora (Police) na Andre Mazimpaka (Mukura VS).

Mabeki; Michel Rusheshangoga (APR), Fitina Omborenga (SC Kiyovu), Celestin Ndayishimiye (Mukura VS), Abouba Sibomana (Gor Mahia, Kenya), Soter Kayumba (AS Kigali), Abdul Rwatubyaye (APR), Emery Bayisenge (APR) na Salomon Nirisarike (Sint-Truidense, Ubelgiji).

Viungo; Yannick Mukunzi (APR), Djihad Bizimana (APR), Jean Baptiste Mugiraneza (Azam, Tanzania), Amran Nshimiyimana (Police), Haruna Niyonzima (Yanga SC, Tanzania), Dominique Savio Nshuti (Rayon Sports), Innocent Habyarimana (Police), Jean Claude Iranzi (APR), Yussufu Habimana (Mukura VS), Muhadjiri Hakizimana (Mukura VS)

Washambuliaji; Ernest Sugira (AS Kigali), Quentin Rushenguziminega (Lausanne Sport, Uswisi), Elias Uzamukunda (Le Mans, Ufaransa) na Dany Usengimana (Police).

Mkwasa Ampa Ushauri Wa Bure Nadir Haroub ‘Cannavaro’
Milutin Sredojevic ‘Micho’ Amjumuisha Kikosini Okwi