Aliyekua Kocha Msaidizi wa Azam FC Vivier Bahati ametambulishwa rasmi na Uongozi wa Biashara United Mara, baada ya kukamilisha mazungumzo ya ajira.

Vivier ametambulishwa Biashara United kama Kocha Mkuu wa klabu hiyo ambayo inapambana kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu 2021/22.

Bahati aliondoka Azam FC sambamba na bosi wake George Lwandamina, kufuatia mambo kuwaendea mrama katika michezo ya mwanzo ya msimu huu 2021/22.

Biashara United Manara ilikua haina Kocha Mkuu tangu alipoondoka Kocha kutoka nchini Kenya Moses Odhiambo.

Msomi wa chuo kikuu alizwa na mwanamke wa 'Instagram'
Jemedari awashukia wadau wa soka