Mabingwa wa kihistoria duniani, timu ya taifa ya Brazil wameendelea kuwasogelea wapinznai wao wa jadi Argentina katika viwango vya ubora wa soka duniani.

Brazil wamepanda hadi kwenye nafasi ya pili, katika viwango vya ubora vya mwezi Novemba hali ambayo inadhihirisha huenda wakarejea katika nafasi ya kwanza endapo watafanya vyema katika michezo itakayowakabili miezi michache ijayo.

Brazil wametinga katika nafasi ya pili na kuwaondoka mabingwa wa sasa wa dunia timu ya taifa ya Ujerumani, ambao wameshuka kwa nafasi moja.

Sifa iliyowapa nafasi Brazil hadi kukwea katika nafasi ya pili ya viwango vya ubora wa soka duniani, ni mafanikio ya ushindi waliyoyapata katika michezo yao sita iliyopita ikiwa ni pamoja na kuwacharaza Argentina mabao matatu kwa sifuri mapema mwezi huu.

Katika orodha ya mwezi Novemba Chile wamepanda na kuzipiku Ubelgiji pamoja na Colombia kwa kushika nafasi ya nne, huku watoto wa malkia Wales na England wakishuka hadi katika nafasi ya 12 na 13.

Timu ya taifa ya Armenia imeonyesha kupiga hatua kubwa katika orodha hiyo kwa kupanda kwa nafasi 38, ambapo sasa ipo katika nafasi 87.

Orodha ya timu kumi bora ambayo imetolewa na FIFA kwa mwezi Novemba.

1.Argentina (1), 2. Brazil (3), 3. Germany (2), 4. Chile (6), 5. Belgium (4), 6. Colombia (5), 7. France (7), 8. Portugal (8), 9. Uruguay (9) na 10. Spain (10)

Orodha kamili bofya hapa

FIFA wanatarajia kutoa orodha nyingine ya viwango vya ubora wa soka duniani itakapofika Disemba 22.

Lionel Messi: FC Barcelona Haitegemei Mtu Mmoja
Magufuli aanika upigaji dili uliobarikiwa na Bodi ya TRA, aimulika TEA