Zikiwa zimebakia siku tatu pekee kabla ya upigaji kura nchini Marekani, mgombea urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton ameungana na mwanamziki wa mtindo wa Rap, Jay Zee katika hafla maalumu inayokusudia kuwahamasisha wapiga kura wenye asili ya Afrika kujitokeza kwa wingi Jumanne kupiga kura.

Kura ya maoni ya sasa inaonyesha kuwa kura yoyote itakayopigwa itatekeleza wajibu muhimu kuamua ni nani atakayeongoza.

Mgombea urais wa chama cha Republic, Donald Trump anaonekana kukaribiana sana na Clinton na hakuna uhakika kuwa ni nani atakayeshindwa kwa wakati huu.

Kwa sasa pande zote zinafanya mikakati ya kuwashauri wapigaji kura kupiga kura baada ya kuwashawishi wale ambao bado hawajafanya uamuzi.

Vugu vugu hilo la uchaguzi likiendelea kupamba moto, mawakili wa chama cha Democratic wameanza kuwasilisha kesi mahakamani wakisema mawakala wa Donald Trump wameanza tabia ya kuhakikisha watu fulani hawapigi kura siku ya upigaji kura.

Jaji wa jimbo la Ohio Marekani, ametoa amri dhidi ya kundi la kampeni la Donald Trump lihakikishe kuwa halishiriki katika kuwatisha watu wanaotaka kupiga kura huku Trump naye ametoa wito kwa mawakili wake watekeleze wajibu wa wachunguzi ili kujiepusha na ulaghai na kuhakikisha mtu haibi kura.

 

 

Wasomi wachambua msimamo wa Magufuli kuhusu katiba mpya
Joto la uchaguzi nchini Marekani lazidi kupanda