Hali ya sintofahamu imezidi kukigubika Chama Cha Wananchi CUF mara baada ya kutwangana makonde mazito katika mkutano wao na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam.

Vurugu hizo ziliibuka dakika chache tu mara baada ya mkutano huo kuanza ndipo lilipojitokeza kundi la vijana ambao walikuwa wameficha nyuso zao kwa kuvalia vitambaa vyeusi usoni na kuanza kuwashambulia viongozi waliokuwa meza kuu.

Aidha, Watu hao wasiofahamika wakiwa na bastola, mapanga na marungu walivamia mkutano wa wanachama wa upande unaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, uliotakiwa ufanyike Mabibo jijini Dar es salaam.

Hata hivyo, Polisi walifika katika eneo hilo na kuwahoji baadhi ya wanachama wa CUF waliovamiwa  katika ukumbi huo.

Mwalimu ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuua
Video: Dakika 10 za damu CUF, Magufuli aitisha kikao cha wabunge wa CCM