Kansa ni ugonjwa unaosababisha ukuaji wa seli ambazo hushambulia mwili kwa namna tofauti tofauti.

Kuna zaidi ya aina 100 za kansa ikiwemo ya matiti, ngozi, ini, mapafu, figo, damu, njia ya uzazi, ovari, na kansa ya ngozi na nyingine nyingi ambazo hazipo kwenye orodha hii na kila kansa ina dalili zake.

Tafiti mbalimbali zilizofanywa na mashirika ya afya zimebainisha kuwa kansa ni ugonjwa wa pili unaosababisha vifo vya watu wengi zaidi duniani na kulingana na takwimu za shirika la afya duniani (WHO), kadiri miaka inavyozidi kuna 70% ya ongezeko la wagonjwa wa kansa.

Uvutaji sigara, unywaji pombe kupita kiasi, miale ya jua, uzito uliopitiliza, kemikali katika vipodozi, umri mkubwa, kula chakula cha moto kwenye chombo cha plastiki, kuanza kushiriki tendo la ndoa mapema na mengineyo zimetajwa kuwa ndio visababishi vikubwa vya ugonjwa wa kansa.

Na kansa zinazoongoza kuua ni kansa ya mapafu, kansa ya maini, kansa ya utumbo mkubwa, kansa ya tumbo na kansa ya matiti, hivyo zifuatazo ni aina ya vyakula ambavyo inashauriwa kuvitumia kwani aina hizi za vyakula viana uwezo mkubwa wa kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya kansa.

1.Chai
Inaelezwa kuwa chai ya kijani na nyeusi ni chanzo kizuri cha kirutubisho kiitwacho ‘catechins’ chenye uwezo mkubwa wa kudhibiti ukuaji wa saratani mwilini. Vile vile chai ina uwezo wa kupunguza hatari ya mtu kupatwa na saratani ya ini, ngozi na tumbo. Taasisi ya Saratani nchini Marekani inaendelea na utafiti kuhusu uwezo wa chai ya kijani na nyeusi katika kupambana na ugonjwa huu hatari usio na tiba.

2. BOGA
Vyakula vingine vinavyotajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia saratani ni Maboga pamoja na karoti, machungwa, viazi vitamu, pilipili nyekundu na za njano. Jamii ya vyakula hivi vina kiwango kikibuwa cha kirutubisho aina ya ‘beta carotene’ na vinapoliwa mara kwa mara vinapunguza hatari ya mtu kupatwa na aina mbalimbali za saratani.

3. SPINACHI
Mboga za majani zenye rangi ya kijani, Spinachi ikiwa inaongoza, ni vyakula ambavyo vina uwezo mkubwa wa kutoa kinga mwilini au kuondoa hatari ya kupatwa na saratani ya ini, kizazi, utumbo mpana na kibofu cha mkojo.

Mboga za majani zinapaswa kuwa katika orodha ya vyakula tunavyokula kila siku, hasa ukizingatia umuhimu wake katika mapambano dhidi ya magonjwa ya kansa na kuwepo kwa kiwango kingi cha Vitamin E, ambayo nayo ni muhimu kwa kinga ya mwili.

4. KITUNGUU SAUMU
Bila shaka kitunguu saumu kinajulikana na kila mtu kutokana na kutumika majumbani karibu kila siku kama kiungo cha mboga. Lakini kitunguu saumu ni zaidi ya kiungo kwani nacho kimeonesha uwezo wa kuondoa hatari ya kupatwa na saratani ya tumbo, koo na matiti kwa mtu anayetumia mara kwa mara. Ili kukiongezea uwezo wake wa kupambana na saratani, kikatekate dakika 10 kabla ya kukipika.

5. NANASI
Nanasi nalo ni chanzo kikuu cha Vitamin C ambayo hutoa kinga mwilini. Mbali na hilo, nanasi pia lina kimeng’enya aina ya ‘bromelain’, ambacho ni muhimu sana katika kutoa kinga dhidi ya saratani ya matiti na mapafu.

6. EPO (apple)
Mbali ya kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa kinga mwilini, Epo lina kirutubisho muhimu kiitwacho ‘quercetin’ ambacho kimeonesha kuwa na uwezo mkubwa wa kupunguza hatari ya mtu kupatwa na saratani ya mapafu na ina uwezo wa kupunguza kasi ya kukua ama kuongezeka kwa seli za kansa ya kibofu. Japo bei ya tunda hili kwa sasa ni shilingi 1000 lakini ni muhimu kwa afya zetu.

Vyakula vyote vilivyoorodheshwa hapo juu, vina uwezo wa kupambana na saratani kwa njia ya kipekee, lakini utafiti umeonesha kuwa yanapoliwa yote kwa pamoja, hutoa kiwango kikubwa zaidi cha kinga. Hivyo basi, pendelea kula vyakula vyenye uwezo mkubwa wa kutoa kinga mwilini dhidi ya saratani, ambavyo ni matunda, mboga na nafaka, huku vikitiliwa mkazo vyakula vilivyoorodheshwa hapo juu.

Thibaut Courtois akacha mazoezi Chelsea
Dkt. Kalemani apiga marufuku TANESCO, REA kuagiza vifaa nje ya nchi