Vyama vya Chadema, ACT Wazalendo na NCCR Mageuzi vimetangaza kugomea kushiriki uchaguzi wa udiwani katika Kata ya Mwanzage jijini Tanga kwa kile walichoeleza kuwa ni kuwepo kwa zuio la mahakama juu ya uchaguzi huo.

Wakizungumza katika mkutano wa pamoja, viongozi hao wamesema mbali na zuio la mahakama lakini hawaoni kama uchaguzi utakuwa wa huru na haki kutokana na kuwepo kwa mazingira yasiyoridhisha ikiwemo ucheleweshwaji wa kuchukua fomu za kugombea.

”Sababu kubwa ni zuio la mahakama linaloonyesha kufanya uchaguzi ni batili, pili katika uchaguzi uliofanyika kata ya Mabokweni haukuwa wa haki pamoja na matumizi makubwa ya nguvu ya dola”, amesema Katibu mkuu wa CHADEMA wilaya ya Tanga Jonathan Baweji.

Naye Mwenyekiti wa ATC Wazalendo, Hamin Kidege ametaja sababu ya chama chao kutoshiriki ni kukosekana kwa uungwana katika chaguzi za kata mbalimbali zilizopita hivyo hawaoni kama katika kata hiyo mambo yamebadilika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi wilaya ya Tanga, Richard Abel amesema chama chake kimeamua kuungana na vyama vingine kujitoa katika uchaguzi huo, kutokana na kupuuzwa kwa agizo la mahakama la kutofanyika kwa uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC), uchaguzi wa udiwani na wambunge katika kata na majimbo yaliyotangazwa utafanyika Septemba 16, mwaka huu.

Ulega atoa maagizo mazito kuhusu tozo za Samaki
Dkt. Mwakyembe ateta na Machifu