Viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani nchini akiwemo Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe na Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara upande wa Maalim Seif, Joel Lwehabura wameonekana kwenye kesi ya dhamana inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe pamoja na Mbunge Ester Matiko.

Mbali na viongozi hao wakubwa pia mahakamani hapo ilishuhudiwa wafuasi wengi wa CHADEMA waliojitokeza kwaajili ya kusikiliza hatma ya kiongozi wao, Freeman Mbowe.

“Tunawaambia wanachama wote kesho saa mbili waje mahakamani, chama chote kitahamia hapa, naomba wanachadema tushikamane kwa ajili ya mwenyekiti wetu,”amesema Meya wa Ubungo Boniface Jacob

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu CUF Bara, Joel Lwehabura amesema kuwa kwa hali ilivyo sasa kuna nguvu ya kutaka kuumiza upinzani, hivyo wameamua kuungana ili wawe na nguvu zaidi.

Mbowe na Matiko wamerudishwa rumande kwaajili ya kusubiri kusikilizwa kwa kesi ya kupewa au kutopewa dhamana, Alhamisi ya wiki hii saa mbili asubuhi.

 

Majaliwa aagiza kukamatwa kwa watumishi waliotafuna bilioni 3
Watumishi watakiwa kuongeza ubunifu