Polisi nchini Kenya imeeleza kuwa vifaa vya Reli ya Kisasa (SGR) vilivyokuwa vimeibwa vimekutwa nyumbani kwa diwani wa Noromoru.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh1 milioni za Kenya, vilikutwa ndani ya nyumba ya Martin Matu baada ya kufanya msako mkali.

Imeelezwa kuwa vifaa hivyo vilikuwa vimeibwa katika ofisi za SGR zilizoko jijini Nairobi.

Diwani huyo anatakiwa kufika katika ofisi ya DCI mapema Jumatatu kwa ajili ya mahojiano kabla ya kufunguliwa mashtaka kamili.

“Diwani Matu ameshaelekezwa kuwa anatakiwa kufika kwenye ofisi za DCI Jumatatu asubuhi, ofisi zilizopo karibu na Reli,” DCI amesema mapema leo.

Akizindua treni ya abiria ya kisasa Mei 2017, Rais Uhuru Kenyatta aliapa kuulinda mradi wa SGR kwa hali yoyote ikiwa ni pamoja na kuruhusu hukumu ya kifo kwa watakaohujumu.

Akizindua treni hiyo ya abiria yenye thamani ya Sh 327 za Kenya jijini Mombasa, Rais Kenyatta alisisitiza kuwa sheria inampa mamlaka ya kuhalalisha utekelezaji wa hukumu ya kifo.

Serikali yaikana kampeni ya Makonda kuhusu mashoga
Wanafunzi wa chuo kikuu wazama mtoni wakijipiga Selfie