Kaimu mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Bukoba, Abdulahiman Ngaugia, amethibitisha kutokea kwa moto ulioteketezaa nyumba mbili zenye vyumba 17 zilizopo katika kambi ya wavuvi ya Igabiro kata ya Kaagya, Bukoba mkoani Kagera

Kamanda Ngaugia, amesema nyumba hizo mali ya Abduswamadu Kalokola na Frederick Mtoka zimeteketea kwa moto jana saa 11:30 jioni na kuwahi eneo la tukio, na kufanikiwa kupunguza madhara kwa kuzima moto huo kabla haujaenea zaidi, katika nyumba nyingine.

Kufuatia tukio hilo ambalo mbali na kuteketeza mali halikusababisha kifo au majeruhi, jeshi la zimamoto na uokoaji baada ya kuzima moto huo, walitoa elimu kwa wakazi wa eneo hilo na kuwataka kuchukua tahadhari ili kupunguza ajali za moto.

Ahueni ya tozo za miamala ya simu
Taliban washerehekea kuondoka kwa Marekani