Kikao kinachohusika na kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa CCM nafasi za ubunge na uwakilishi kwaaajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 hakitoweza kufanya uteuzi wa wakilishi na kufanya uteuzi wa ubunge na viti maalum ubunge kutokana na ratiba ya tume za uchaguzi za NEC na ZEC kupishana katika hatua za uteuzi.

Hayo yamesemwa leo Tarehe 20 Agusti 2020 na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Bashiru Ally katika mkutano wa uteuzi wa nafasi za ubunge na uwakilishi jijini Dodoma.

Amesema kwa mujibu wa katiba idadi ya akidi ni 167, na akidi inatakiwa iwe na wajumbe nusu ambao ni 84 lakini wajumbe 54 kati yao 42 ni ubunge na 12 ni wawakilishi hawatakuwa kwenye kamati ya uteuzi kutakana na kanuni na sheria za mgombea kuwa ndani ya kamati.

Kati ya maakidi 110 wawili ndiyo wenye udhuru na kupelekea kuwa na maakidi 108 na kuthibitisha kwa mwenyekiti wa CCM kuwa ni mkutano sahihi

“Watakaoteuliwa ndio watakao peperusha bendera ya CCM kutetea chama chetu kuwa na wabunge wengi katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”. Amesema Bashiru.

Bwalya afurahia anachokiona Simba SC
JPM: Nimepitia majina yote ya watiania