Madereva bodaboda zaidi ya 100, wameandamana hadi ofisi za Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara, ACP Longinus Alexander Tibishubwamu wakifurahia na kuwapongeza Askari Polisi kwa kufanikiwa kudhibiti matukio ya ujambazi wa kutumia silaha mkoani humo.

Katika tamko lao, lililosomwa na Afisa Habari wa Umoja wa Madereva Bodaboda Mkoani Mara, Faustine Mbaruku hii leo Septemba 28, 2022 wamesema mbali na hongera hizo pia wanalitaka Jeshi la Polisi nchini kuendelea na udhibiti huo wa uhalifu hali iliyoongeza ari ya ufanyaji wa kazi kwa nyakati zote.

Wamesema, “Nani asiyejua kwa kipindi cha hivi karibuni hakuna kijana wa bodaboda aliyekua anajua kesho ataamka akiwa hai au ataamka akiwa hana jeraha katika mwili wake au akiamka akiwa na bodaboda yake, hali hii ilitupelekea kuteteresha ustawi wa familia zetu.”

Awali, Mwenyekiti wa waendesha Boda Boda Mkoa wa Mara, alitumia nafasi hiyo kuzungumzia mikasa ya ujambazi na uhalifu wa silaha za moto, ambao wananchi wa mkoa huo wamekutana nayo haswa madereva wenzake na kusema kwasasa wanaishi salama wao na familia zao.

Moja ya mambango yenye ujumbe katika maandamano ya amani ya kulipongeza Jeshi la Polisi Mkoani Mara kwa kudhibiti uhalifu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ACP Longinus Alexander Tibishubwamu amewapokea Madereva hao na kuwapongeza kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa kwa Jeshi la Polisi, katika kuwafichua wahalifu na kuwaahidi kuendeleza jukumu la misingi ya ulinzi wa raia na mali zao.

Amesema, “Niwahakikishie kuwa sisi tuko pamoja na nyinyi, tunatambua shughuli zenu za usafirishaji katika uje zi wa Taifa, hivyo tunawahakikishia kwamba mtaendelea kufanya kazi masaa 24, mawasiliano yetu mnayo hivyo kunapotokea viashiria vyovyote vya uhalifu msisite kutufahamisha na tutafika haraka kudhibiti hali hiyo.”

Zanzibar 'yajifagilia' mazingira bora uwekezaji
Dejan: Mkataba wangu umevunjwa Simba SC