Maandamano dhidi ya Serikali, ambayo ni makubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Irani tangu 2009, yanayoongozwa na jamii ya Wakurdi wa Oshnavieh yameenea na kufikia miji 80 na kusababisha waandamanaji hao kuuteka mji mdogo, .

Mamlaka za nchi hiyo, zimekuwa zikiyakabili maandamano hayo kwa kutumia nguvu ambapo siku ya Ijumaa (Septemba 23, 2022), vyombo vya habari vya serikali vilisema watu 35 wameuawa, lakini mashirika ya haki za binadamu yanasema idadi ni kubwa zaidi.

Katika maandamano hayo, Wanaharakati na waandishi wa Habari pia wamekamatwa na inaarifiwa kuwa mbali na sheria kali za kiislamu, pia kuna na malalamliko mengi juu ya ufisadi, usimamizi mbaya wa kiuchumi na ukandamizaji mkubwa wa kisiasa.

Chanzo cha muendelezo wa maandamano kinatokana na kifo cha msichana Mahsa Amini (22), ambaye alikamatwa na Polisi wa maadili kwa tuhuma za kukiuka agizo la hijabu, ambalo linahitaji kufunika nywele na kutovaa nguo za kubana kwa wanawake.

Kufuatia hali hiyo, Wanawake wengi wa nchi hiyo wameongoza maandamano hayo kwa kuchana vitambaa vyao vya kichwa, kuvipunga kwa mikono na kuvichoma huku wanaume wakishangilia.

Inaarifiwa kuwa, chuki imekuwa ikijengeka kwa miezi kadhaa kutokana na ukandamizaji ulioamriwa Rais wa Iran Ebrahim Raisi ambaye anatajwa kuwa na misimamo mikali, ukiwalenga wanawake.

Kocha Mgunda: Primeiro de Agosto wanatumia nguvu, akili nyingi
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 26,2022