Idara ya Habari na Mawasilino ya Young Africans imewashukia baadhi ya Waandishi wa Habari na Mashabiki wa Soka la Bongo wanaoizungumzia kwa mazuri na kuipamba klabu ya Al Hilal ya Sudan na kuacha kusema mazuri ya Wananchi (Yanga SC).

Young Africans itaikaribisha Al Hilal Jumamosi (Oktoba 08), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kisha itakwenda mjini Khartoum-Sudan kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili kati ya Oktoba 14-16.

Akihojiwa na Wasafi FM mapema leo Alhamis (Septemba 29), Mkuu wa Idara hiyo Ally Kamwe, amesema anashangaa kuona Al Hilal inapewa nafasi kubwa kuzunguzwa katika baadhi ya Vyombo vya Habari na katika Mitandao ya Kijamii, lakini Young Africans inaachwa.

“Young Africans ni Timu bora Tanzania, tuna Squad ambayo imekwenda unbeaten michezo 41 ya Ligi, Hii rekodi angekuwa nayo Al Hilal, Young Africans tusingelala.”

“Lakini watu hawawaambii kama wanakuja kucheza na Dubwasha ambalo limecheza michezo 41 bila kufungwa, na hiyo michezo 41 wapambe wenu wapo”

“Tunaporeport Al Hilal tureport pia na ukubwa wa Young Africans, ukubwa ambao tuko nao,” amesema Kamwe

Al Hilal ilisonga mbele katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa faida ya bao la ugenini dhidi ya Mabingwa wa Soka wa Ethiopia St George, ikitanguliwa kufungwa 2-1 ugenini na kushinda nyumbani Khartoum-Sudan 1-0.

Young Africans ambayo ndio Bingwa wa Tanzania Bara, ilisonga mbele kwenye Michuano hiyo kwa kuibamiza Zalan FC kutoka Sudan Kusini kwa matokeo ya jumla 9-0. Ikishinda 4-0 kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza, kisha ikashinda 5-0 katika mchezo wa Mkondo wa Pili.

Ibrahim Class: Sitamdharau Gustavo Pina Melgar
Ally Kamwe: Lengo ni kucheza Robo Fainali