Mahakama nchini Myanmar imetupilia mbali hoja inayotaka kufutwa kesi dhidi ya waandishi wawili wa shirika la habari la Reuters waliotiwa mbaroni wakati wakichunguza mauaji dhidi ya Waislamu wa jamiii ya Rohingya.

Waandishi hao wa habari, Lone mwenye umri wa miaka 32 na Kyaw Soe Oo mwenye umri wa miaka 27, walitiwa mbaroni Desemba mwaka jana kwa tuhuma za kukiuka sheria za nchi hiyo inayohusiana na taarifa za siri za nchi zinazohusiana na operesheni za kiusalama katika jimbo lililo kumbwa na mgogoro la Rakhine.

Aidha, Waandishi wa habari, Lone na Kyaw Soe Oo, walitiwa mbaroni Desemba wakituhumiwa kwa kukiuka sheria ya nchi hiyo inayohusiana na taarifa za siri za nchi zinazohusiana na operesheni za kiusalama katika jimbo lililo kumbwa na mgogoro la Rakhine.

Hata hivyo, Waandishi hao wawili wa habari walikuwa wakichunguza mauaji ya watu 10 wa jamii ya Rohingya yaliyofanyika Septemba 2 katika kijiji cha Inn Din kilichoko katika jimbo la Rakhine yanayodaiwa kufanywa na vikosi vya usalama pamoja na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho.

Mugabe awekwa kikaangoni
Video: Ripoti ya CAG yawaweka kona mawaziri watano, Waziri Ummy ataka faragha kwa Makonda

Comments

comments