Zikiwa zimesalia siku chache, kabla ya raia nchini Kenya kupiga kura katika uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu, tayari mashirika ya kiraia ya ndani na yale ya kimataifa yameanza kufuatilia mchakato wa uchaguzi huo.

Ikumbukwe kuwa, mwaka 2017 mahakama ya juu ilifuta uchaguzi huo kwa dosari zilizojitokeza, na kusambazwa kwa waangalizi kama ilivyo kwa umoja wa Ulaya, ni kujaribu kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani.

Tayari, umoja wa ulaya umetangaza kutuma waangalizi 180, ambapo 48 tayari wamewasili, huku gharama za waangalizi hao zikitajwa kufikia euro milioni 8.

Baadhi ya Wananchi katika uhamasishaji wa kampeni za amani nchini Kenya.

Kiongozi wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya, Ivan Shtefanek amezungumzia hatua ambazo wamezipiga kwa sasa na kusema wataendelea kufuatilia hadi baada ya uchaguzi huo wanaotaraji utakuwa huru na haki.

“Tumeanza kufuatilia kampeni, na tutaendelea kufuatilia hadi baada ya uchaguzi, siku ya uchaguzi tutaangalia ufunguzi wa vituo, upigaji kura pamoja na utangazaji matokeo na tunaamini utakuwa huru na wa kuaminika.” amesema Ivan Shtefanek.

Hata hivyo, tayari waangalizi hawa wameonesha masuala kadhaa ambayo ni lazima tume ya uchaguzi iyaangalie kwa umakini. Beata Martin Ruzo-Milo-Vich, naibu kiongozi wa waangalizi kutoka umoja wa Ulaya kwa upande wake naye ameelezea mipango yao kuelekea uchaguzi huo.

Kampeni za uchaguzi nchini Kenya.

 “Tutafuatilia hatua zote za uchaguzi ambazo raia wa Kenya wana wasiwasi nazo, na hii inaanzia katika kuheshimu sheria, sajili ya wapigakura na hata kampeni,” amesema.

Ameongeza kuwa, pia wataangalia mchango wa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, pamoja na matumizi ya teknolojia kwa ajili ya uchaguzi na mchango wa wanawake na makundi mengine.

Waziri aungana na timu kufuatilia ugonjwa usiofahamika
Joto Mediterania lasababisha vifo 238