Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF, limetoa oridha ya waamuzi watakaochezesha mchezo wa mzunguuko wa pili wa hatua ya makundi, kombe la shirikisho kati ya Young Africans dhidi ya Rayon Sports kutoka Rwanda.

CAF imewateua waamuzi kutoka nchini Angola kuchezesha pambano hilo, ambalo litaunguruma uwanja wa Taifa Dar es salaam, mwishoni mwa juma lijalo.

Kaimu afisa Habari wa shirikisho la soka nchini TFF Clifford Mario Ndimbo, amesema tayari orodha ya waamzi hao imeshatumwa nchini na kupokelewa na katibu mkuu Wilfred Kidao.

Waamuzi hao ni Helder Martins Rodrigues De Carvalho (Mwamuzi wa Kati) Ivanildo Meireles De O Sanche Lopes (Mshika Kibendera namba 1), Wilson Valdmiro Ntyamba (Mshika Kibendera namba 2), Joao Amado Muanda Goma (Fourth Official) wote wakitokea Angola.

Maafisa wengine ni Abebe Solomon Gibresilassie (Commissioner) (Ethiopia), Yoland Mavouroulou (General Coordinator) (Gabon) na Clifford Mario Ndimbo (Media Officer) Tanzania.

Laurent Koscielny kusubiri hadi Disemba
Mwakyembe azindua Baraza la Michezo la Taifa la Kumi na nne

Comments

comments