Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF limewateua waamuzi kutoka nchini Algeria kuchezesha pambano la kuhitimisha ratiba baina ya Tanzania na wenyeji Nigeria.

Waamuzi watakaochezesha pambano hilo ni Mehdi Abid Charef atakayesimama kati, akisaidiwa na waalgeria wenzake, Abdelhak Etchiali na Ahmed Tamen huku mwamuzi wa akiba akiwa. I Mustapha Ghorbal.

Kamishna wa mchezo atakuwa Inyangi Bokinda kutoka JK Kongo. Pambano hilo la kundi G la mbio za kuwania kufuzu Kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika litachezwa tarehe 3 mwezi Septemba katika uwanja wa Adokiye Amiesiamaka mjini Port Harcout, Nigeria.

Pambano la awali lililochezwa jijini Dar mwaka jana lilimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Rio Olimpiki 2016: Rekodi Iliyodumu Kwa Miaka 48 Yavunjwa
Frank de Boer Azima Moto Kwa Petroli, Abisha Hodi Stadio San Paolo