Kundi la Mawakili wanaoishi London wamefungua shauri kwa niaba ya mamia walioathiriwa na ndugu waliouawa kwenye vita nchini Yemen katika Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC, wameitaka Mahakama hiyo kufanya uchunguzi kuhusu vitendo vya uhalifu wa kivita vinavyo daiwa kufanywa na wanajeshi wanaoungwa mkono na Serikali.

Kundi hilo la mawakili linalojulikana kama Guernica 37, limewasilisha ushahidi kwenye Mahakama ya ICC kwa kuonesha vitendo vya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Yemen uliofanywa na vikosi vya usalama.

Umoja wa Mataifa umeelezea kuwa hali ya nchini Yemen imekuwa mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani. wakati wataalamu wa Umoja huo wakizishtumu pande zinazohasimiana kwa uhalifu wa kivita.Serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa, imekuwa ikipambana na waasi wa Kihouthi wanaoungwa na Iran tangu mwaka 2014

Nahodha wa Zamalek aadhibiwa
UN yakuna kichwa kuzikwamua kiuchumi nchi masikini kutokana na Corona