Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekubaliana kuwa wabunge wake wote wanaoshiriki michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)  kuondoka mara moja kwenye kambi ya timu ya Tanzania.

Chadema kimeazimia amuzi hilo katika kikao chake cha dharura kinachoendelea ambacho kiliitishwa kwa lengo la kutafakari kwa kina maendeleo ya hali ya siasa nchini.

Chama hicho kimesema kuwa maagizo hayo yameanza kutekelezwa usiku wa Jumatano, Disemba 6 mwaka huu baada ya kupitishwa kwa azimio hilo ambapo Kamati Kuu ilimuagiza Katibu wa Bunge kuwafikishia wabunge wahusika mara moja.

Baada ya kupokea tathmini ya kina ya Uchaguzi wa marudio katika Kata 43 uliofanyika hivi karibuni Chadema kimebaini kuwa ulitawaliwa na uvunjifu Mkubwa wa Haki za binadamu.

Aidha Chadema kimesema kuwa maazimio mengine ya kikao cha Kamati Kuu ambacho kinaendelea jijini Dar yatatolewa katika hatua ya baadae ambapo umma utaarifiwa rasmi.

Mwalimu amkung'uta makonde Mwalimu Mkuu
Diamond Platinumz ft Rick Ross, video ipo tayari ''Waka''