Sakata la uenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) limechukua sura mpya baada ya wabunge wa chama hicho kueleza kuwa wamenasa njama zinazoandaliwa na Profesa Ibrahim Lipumba kutaka kukivuruga chama hicho na kurejea ofisini kwa nguvu hivi karibuni.

Wabunge hao ambao wamepinga uamuzi wa Profesa Lipumba kutaka kurejea kwenye nafasi ya uenyekiti baada ya kujiuzulu mwaka jana, wameeleza kubaini njama za Profesa Lipumba kukivuruga chama hicho kupitia ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge wa chama hicho, Riziki Shahari alisema kuwa Profesa Lipumba amewapanga wafuasi wake kumpokea katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho yaliyoko Buguruni jijini Dar es Salaam wakiwa na fulana zenye jumbe mbalimbali, na kwamba kinachosubiriwa ni msajili kumtangaza Profesa Lipumba kama Mwenyekiti halali.

“Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi asikubali kuvunjiwa heshima yake kubwa akiwa Jaji aliyehudumu katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa muda mrefu,” alisema Mbunge huyo.

Alionngeza kuwa wamebaini kuwa Lipumba amejipanga kupitia njama hiyo, kuzungunguka nchi nzima akifanya vikao vya ndani katika kile walichokiita ‘jaribio la kuimaliza kabisa CUF’.

Shahari alisema kuwa Katiba ya chama hicho hairuhusu mwenyekiti aliyejiuzulu kutengua maamuzi yake na kurejea tena.

Profesa Lipumba aliwasilisha barua katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa akipinga uamuzi wa Baraza Kuu la chama hicho kumsimamisha uanachama. Hali hiyo ilipelekea Msajili kuitaka CUF kuwasilisha kwake ufafanuzi wa hatua zilizopitiwa kufikia maamuzi hayo dhidi ya Profesa Lipumba.

Kilimanjaro : Ajiua baada ya kuhukumiwa miaka 60 jela
UVCCM wavurugana Arusha