Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson amewataka Wabunge wapya wa Bunge wa Afrika Mashariki (EALA), waliochaguliwa hapo jana Septemba 22, 2022 kutumia nafasi ya kuwawakilisha vyema wananchi wa Tanzania katika kufikisha na kuzitatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Hatua ya Dkt. Tulia inafuatia kutangazwa kwa wabunge tisa walioibuka na ushindi kwenye uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki(EALA), kati ya Wagombea 20 waliokuwa wakichuana kuwania nafasi hiyo Bungeni, Jijini Dodoma.

East African Legislative Assembly. (EALA). Picha na eala.org

Awali, akitangaza majina ya washindi hao Spika Dkt. Tulia amewataka Wabunge hao kwenda kuliwakilisha Vyema Taifa katika Bunge la Afrika Mashariki kama ambavyo wameahidi kwenye Kampeni zao.

Washindi hao ni Angella Kizigha(CCM), Nadra Mohammed(CCM), Dkt. Shogo Richard Mlozi (CCM), Abdulla Hasnuu Makame (CCM), Machano Alli Machano (CCM), Mashaka Khalfan Ngole (CUF), Ansari Abubakar Kachwamba (CCM), James Kinyasi Millya, (CCM) na Dkt. Ng’waru Jumanne Magembe (CCM).

Djigui Diara atuma salaam kwa Mashabiki Young Africans
Kocha Big Bullet awaangukia mashabiki Malawi