Wabunge wa Chama tawala Nchini Uganda cha National Resistance Movement (NRM) cha Rais wa sasa wa nchi hiyo, Yoweri Museveni wamekubaliana kuwasilisha bungeni mswada wa kuondoa ukomo wa umri wa rais kutoka kwenye katiba ya nchi hiyo.

Katiba ya Uganda kwa sasa hairuhusu mtu yeyote mwenye umri zaidi ya miaka 75 kugombea nafasi ya urais wa nchi hiyo ili kutoa wigo kwa vijana ambao bado wana nguvu za kuweza kulitumikia taifa lao.

Aidha, Rais wa sasa wa nchi hiyo, Yoweri Museveni ana umri wa miaka 73, ambapo ni miongoni mwa viongozi waliotawala kwa muda mrefu zaidi barani Afrika na amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo mitatu.

Hata hivyo, Uchaguzi Mkuu wa Urais nchini humo unatarajiwa kufanyika mwaka wa 2021 ambapo rais wa sasa atakuwa ameshavuka miaka kadhaa umri huo.

Australia kucheza na Syria mjini Melecca
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Septemba 14, 2017