Wabunge wanane waliofukuzwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, anayetambuliwa na Msajili wa vyama vya Siasa nchini, Prof Ibrahim Lipumba, jana waliondoka vichwa chini baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam kutupilia mbali ombi lao la zuio la kupinga kuapishwa kwa wabunge wapya.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji wa mahakama hiyo, Lugano Mwandambo baada ya kusikiliza hoja zote za pande mbili, ambapo amesema kuwa mahakama imetupilia mbali hoja za walalamikaji za kuweka pingamizi kutaka wabunge wapya wasiapishwe mpaka kesi ya msingi isikilizwe.

Aidha, Mwandambo amesema kuwa mahakama itasikiliza pingamizi la walalamikaji walilofungua kupinga kufukuzwa uanachama wa chama cha wananchi CUF na mwenykiti wao Prof. Ibrahim Lipumba.

Hata hivyo, katika maombi yao walalamikaji wanaomba kutoapishwa kwa wabunge wanane walioteuliwa na kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuziba nafasi zilizoachwa wazi na wabunge hao kwa mujibu wa katiba.

 

McGregor atamba ‘atakavyompasua’ Mayweather ndani ya raundi mbili
Chid Benz awekwa chini ya uangalizi wa Polisi, Mahakama