Wabunge wa vyama vya upinzani wameendeleza kile walichokiahidi ambapo leo asubuhi wametoka nje ya Bunge kupinga Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kuendesha kikao hicho.

Wabunge hao walitoka nje majira ya saa 3 kamili kwa pamoja na kuwaacha wabunge wa CCM pekee, ikiwa ni dakika chache baada ya kusomwa dua maalum ya kuliombea Bunge na Taifa kwa ujumla.

Wabunge hao waliazimia kutohudhuria vikao vyote vya Bunge vitakavyoendeshwa na Dk. Tulia kwa madai kuwa amekuwa akiwakandamiza na kuvunja kanuni ili kuwabana wapinzani.

Sakata hilo lilipata nguvu zaidi baada ya Naibu Spika kukataa hoja ya Mbunge wa Joshua Nassari (Chadema) kutaka Bunge lilisishe shughuli zake kwa muda na kujadili suala la kufukuzwa kwa wanafunzi zaidi ya 7000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma ndani ya saa 24.

Kadhalika, wabunge saba wa vyama vya upinzani wamepewa adhabu mbalimbali za kutohudhuria vikao vya Bunge baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Mamlaka ya Bunge kuwakuta na hatia ya kuhusika katika vurugu zilizotokana na kudai vikao vya Bunge kurushwa Live na TBC1, Januari 27 mwaka huu. Adhabu ambayo wameiita ya kiuonevu.

Rais Shein awafyatua CUF, asema hawezi kuondolewa madarakani kwa kuroga
Dwight Yorke: Mourinho Atawakuputisha Wengi Man Utd