Wabunge Kutoka Vyama vya Upinzani Nchini wamesusia kuhudhuria kuapishwa kwa wabunge saba wa Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi (CUF) katika mkutano wa nane wa Bunge la 11 ulioanza leo kwa madai hawakufurahishwa na maamuzi ya kufukuzwa wabunge 8 wa Viti Maalumu wa chama hicho.

Katika mkutano huo  ulioanza leo Mjini Dodoma na moja ya mambo yaliyopangwa  kwenye ratiba ya mkutano huo ni kuapishwa kwa wabunge wapya 8 wa Viti Maalumu ambao wameteuliwa kuziba nafasi za wabunge 8 wa Viti Maalumu waliofukuzwa uanachama wa chama hicho.

Aidha, Wabunge ambao wamekula kiapo cha uaminifu leo Septemba 5 ni pamoja na  Alfredina Kaigi, Kiza Mayeye, Nuru Bafadhili, Rukia Kassim, Shamsia Mtamba, Sonia Magogo na Zainab Amir.

Hata hivyo, baada ya kumalizika kwa uapisho wa Wabunge hao wa CUF, wabunge wa upinzani waliingia bunge huku  Spika Job Ndugai, akiwapiga kijembe cha kuhoji kwanini walikuwa wamevaa nguo nyeuzi wote.

 

 

Dele Alli hatarini kuzikosa fainali za kombe la dunia 2018
Ufisadi waponza mkataba Mlimani City