Katibu wa Bunge la Tanzania amesema baada ya Job Ndugai kujiuzulu nafasi ya Uspika kwa sasa taratibu za uchaguzi wa kujaza nafasi hiyo zinaendelea na kwamba kwa mujibu wa sheria kiti cha Spika kinapokuwa wazi hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge isipokuwa Uchaguzi wa Spika.

Katibu huyo wa Bunge amesema Kamati zilizokuwa zikutane kianzia January 10,2022 na January 17,2022 hazitokutana kwa wakati huo na badala yake zitakutana wakati wa Mkutano wa Sita wa Bunge February 1-11, 2022 kwa utaratibu wa tarehe zitakazotangazwa na hivyo Wabunge wameombwa kufika Dodoma January 31,2022.

Nadia Mukami amjibu Jalango, ujauzito wa siri
Dkt. Biteko: Msiwatenge wachimbaji wanawake