Viti vya wabunge wa CHADEMA vikiwa Wazi Bungeni

Mapema leo hii ilishuhudiwa Bungeni Jijini Dodoma viti 18 vya wabunge wanawake waliovuliwa uanachama wa CHADEMA vikiwa wazi huku kukiwa na maswali kadha wa kadha na hatimae wabunge hao wameonekana wakitinga katika Baraza kuu la Chama hicho.

Halima Mdee na wenzake 18 waliovuliwa uanachama na Chadema kwa kosa la kujitokeza bungeni kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum kinyume na maagizo ya chama hicho, leo Jumatano Mei 11, 2022 wamefika katika kikao cha Baraza Kuu la chama hicho Mlimani City, Dar es Salaam.

Awali kulikua na taarifa kuwa wabunge wameitwa na Baraza kuu ili kujibu maswali kuhusu uwepo wao Bungeni ikiwa inatafsiriwa na Chama kama utovu wa Nidhamu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema Baraza Kuu litakuwa na ajenda tano ambayo ni mpango mkakati wa chama kwa miaka tano pamoja na mpango kazi wa mwaka.

Mrema alisema ajenda nyingine itakuwa ni rufaa ya nidhamu iliyokatwa na wabunge 19 wa viti maalumu wakiongozwa na Halima Mdee wakipinga kuvuliwa uanachama na kamati kuu ya chama hicho iliyoketi mwisho mwa mwaka 2020.

MOI yapewa siku 14 kutengeneza mashine za MRI na CT-SCAN
PANYA ROAD watikisa Baraza la Madiwani Biharamulo