Wabunge wa Afrika Kusini wamepigana ngumi kufuatia varangati iliyotokea baada ya Spika wa Bunge kuwaamuru maafisa wa usalama kuwaondoa kwa nguvu wabunge wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF).

Amri hiyo ya Spika wa Bunge ilikuja baada ya wabunge hao wa upinzani kupiga kelele na kuzomea wakati Rais Jacob Zuma alipoingia bungeni humo kwa lengo la kulihutubia.

Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Rais Zuma kulihutubia  Bunge hilo tangu mahakama imkute na hatia katika kesi za ubadhirifu wa mali za umma na usimamizi mbaya. Wabunge wa upinzani wanashinikiza Rais huyo ajihudhuru.

Hata hivyo, kura ya kukosa imane na Rais na kumuondoa madarakani ilishindwa kufanikisha nia hiyo ya wapinzani kutokana na wingi wa wabunge wa chama tawala ambao walimpigia kura ya kuwa na Imani naye.

Ijumaa iliyopita, Mahakama ya juu ya Afrika Kusini iliamua kuwa rais Zuma anapaswa kufikishwa kizimbani kufuatia kesi za ufisadi dhidi yake. Rais Zuma amekanusha madai ya ufisadi dhidi yake, lakini alikiri kutumia fedha za umma kufanya ukarabati wa jumba lake la kifahari na aliomba radhi.

Rungu La FA Kuzishukia Spurs, Chelsea, Dembele
Dk. Migiro ateuliwa Balozi Uingereza