Wabunge Kavejuru Felix wa jimbo la Buhigwe na Dkt. Florence Samizi wa jimbo la Muhambwe wameapishwa mapema leo Bungeni Dodoma, baada ya kushinda katika uchaguzi mdogo.

Wabunge hao wanaziba nafasi zilizoachwa wazi kufuatia kifo cha Mbunge wa Muhambwe, Atashasta Nditiye na Uteuzi wa aliyekuwa Mbunge wa Buhigwe Dkt Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uchaguzi huo mdogo ulifanyika Jumapili Mei 16, 2021.

Aidha, Katibu mpya wa Bunge, Nenelwa Mwihambi ameanza rasmi shughuli za Bunge akiwa Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo tangu Chombo hicho cha kutunga sheria kianzishwe mwaka 1925.

Wanariadha 21 wafariki China
Tanzania kupeleka timu nne CAF