Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamehoji maswali ambayo hivi karibuni yalikuwa miongoni mwa hoja za Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa alipokuwa akizungumzia utawa la wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli.

Wakizungumza katika semina iliyofanyika jana katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, iliyoendeshwa na Dk. Haji Semboja kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Harold Sungusia wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wabunge hao walihoji kuhusu Sheria inayompa Rais Mamlaka ya kubadilisha matumizi ya fedha zilizokuwa zimepishwa kwenye Bajeti ya Bunge.

Hamidu Bobali ambaye ni Mbunge wa Mchinga, aliomba kupewa ufafanuzi baada ya kuhoji kuhusu Mamlaka ya Rais katika kubadili matumizi ya fedha ambazo zilipitishwa na Bunge na kupeleka katika maeneo mengine. Rais aliahirisha sherehe za Uhuru na Muungano na kuelekeza fedha zilizokuwa zimepangwa zitumike katika upanuzi wa barabara za Morocco-Mwenge jijini Dar es Salaam na Ghana-Airport jijini Mwanza.

Naye Mbunge wa viti Maalum, Lucia Mlowe aliomba kupewa ufafanuzi kuhusu suala hilo huku akidai kuwa hivi sasa anaona Serikali imekuwa ndiyo inayolisimamia Bunge badala ya Bunge kuisimamia Serikali.

Mlowe alieleza kuwa Rais kubadili matumizi ya fedha zilizotengewa bajeti na Bunge ni kuingilia mhimili mwingine na kwamba hivi sasa anaona mihili ya Bunge na Mahakama haina nguvu bali inasimamiwa na Serikali.

“Ni namna gani wabunge tunaweza kuisimamia Serikali kama hamna uwiano kati ya mihimili hii mitatu?” alihoji.

Akitoa ufafanuzi kuhusu hoja na maswali ya wabunge hao Dk. Semboja alitaja ibara ya 137 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa inampa Mamlaka hayo Rais. Alifafanua kuwa Rais hajakosea kubadili matumizi ya fedha hizo bali taarifa ya matumizi yake inapaswa kupelekwa Bungeni.

Kwa upande w Harold Sungura ambaye ni mwanasheria, alisema kuwa Rais anauwezo wa kufanya maamuzi yoyote kwa fedha za bajeti isipokuwa kwa fedha zilizo kwenye mfumo hodhi (Consolidated fund).

Stewart Hall Afichua Siri Ya Ushindi Dhidi Ya Warabu
Picha: Manny Pacquiao Amshinda Brandley, Ampiga Chini mara mbili