Wabunge nchini Rwanda wamepitisha mswada wa sheria unaoruhusu Mwananchi kupata kibali cha kumiliki na kutengeneza silaha na pia kwa wafanyabiashara kuziuza kwa sharti moja la mmiliki kutokuwa na rekodi yeyote ya uhalifu na uchunguzi mkali kufanyika juu ya taarifa za nyuma.

Ikiwa nchini Marekani mtu kumiliki silaha ni kitendo cha kuwa na kitambulisho tu hali hiyo ni tofauti nchini Rwanda ambapo anayetaka kumiliki silaha anatakiwa awe mwenye akili timamu na mtu ambaye hajawahi kufungwa jela kwa zaidi ya miezi sita.

Ambapo kuhakikisha kuwa mtu huyo yupo vyema na mwenye akili timamu wa kumiliki silaha Serikali imesema ni lazima awe na cheti kutoka kwa daktari wa serikali kuthibitisha uzima wa mtu huyo japokuwa wanasheria wamesisitiza kuangalia zaidi historia ya nyuma ya mtu huyo kuliko kutumia cheti cha utimamu.

Mswada huo wa sheria ambao ukipitishwa utakuwa mbadala wa sheria ya silaha ya Mwaka 2009, utaruhusu Mwananchi kumiliki silaha kwa ajili ya uwindaji, michezo na kujilinda mwenyewe kama mwananchi atafikia vigezo vilivyowekwa kwenye sheria

Na tayari wameanza kupitisha mswada huo ambao utaamua taratibu za upatikanaji, umiliki, ubebaji, utengenezaji, uhifadhi wa aina zote za silaha

Rwanda inakaribia kuruhusu Wananchi kumiliki silaha huku baadhi ya nchi kama Marekani pameshuhudiwa vifo vingi vinavyotokea baada ya watu kupigwa risasi na kutolewa wito wa kubadili sheria ya kumiliki silaha

Argentina yaibamiza Haiti, Messi atamba
Marco Silva kutua Goodison Park

Comments

comments