Kamati ya Bunge inayosimamia hesabu za Serikali nchini Kenya imetoa siku 60 kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi wa kina kwenye Mamlaka ya Usambazaji wa Dawa nchini humo baada ya kutilia shaka matumizi ya mabilioni ya fedha za kupambana na ugonjwa wa covid-19

Spika wa Bunge la Taifa la Kenya, Justin Muturi amesema kuwa bunge hilo litashiriki ipasavyo katika kuhakikisha kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya kupambana na covid-19 zimetumika ipasavyo, na wabadhirifu wanawajibishwa.

Kamati hiyo ya Bunge imeeleza kuwa inataka maelezo ya kina na kupewa taarifa za mara kwa mara kutoka kwa Mkauzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali kuhusu matumizi ya mabilioni hayo ya shilingi za Kenya.

“Tunatoa ukomo wa siku 60 kuanzia leo ili tupate taarifa kamili kuhusu ukaguzi…ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tunatarajia kupata ripoti ya awali,” Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa Unguja, Opiyo Wandayi amekaririwa na Citizen TV.

Kamati hiyo imeelekeza uchunguzi huo uangazie pia tuhuma za rushwa na ufisadi na kuhakikisha kuwa wakenya wanafahamu ukweli.

Kamanda Muroto aeleza chanzo cha basi la Allys kuteketea kwa moto

Rwanda yamsaka ‘mpelelezi wake’ kwa tuhuma za mauaji ya kimbari

Ajira: Makampuni 10 yatangaza nafasi za kazi, ziko hapa
Video: Kamanda Muroto aeleza chanzo cha basi la Allys kuteketea kwa moto